Mkoma Foundation - Home

 
ein Bild

Wapendwa wanafamilia wa Mkoma na jamii kwa ujumla, Nawasalimia katika jina la Bwana Wetu Yesu Kristo.

Ninachukua fursa hii kuwakaribisha katika tovuti hii ya Mkoma Foundation. Mkoma Foundation ilianzishwa wakati wa Pasaka ya mwaka 2006, wakati Mzee Mkoma alipoitisha mkutano wa watoto wake wote huko Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa na nia njema ya kuwaunganisha watoto wawe na umoja na ushirikiano wa shughuli zao za kifamilia, kimaendeleo pamoja na kusaidiana wakati moja wa wanafamilia anapopatwa na matatizo.

Mkutano ulikuwa na mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Mkoma Foundation. Mkoma Foundation bado ni changa na inahitaji mchango mkubwa wa mawazo ya jinsi ya kuiendeleza. Lakini pia, naona ni jambo jema kueleza angalau kwa kifupi lengo hasa la Mkoma Foundation.

Mkoma Foundation imeanzishwa hasa kusaidia ukoo wa Mkoma, waliooa na kuolewa katika ukoo huo na wazaliwa wa ukoo huo katika maswala ya maendeleo na ya kijamii. Kati ya hao waliotajwa hapo, wanaweza kunufaika na Foundation kwa kuwezeshwa kusoma, kuanzisha miradi ya biashara au kwa jambo lolote ili mradi linaleta tija katika familia. Pia, Mkoma Foundation iko kwa ajili ya kuwasaidia wanajamii wa Mkoma katika maswala kama ya ugonjwa na misiba. Kwa vile wana-Mkoma hawaishi peke yao bali na jamii kwa ujumla, hivyo, Mkoma Foundation inaweza kuanzisha miradi ya kijamii kama vile kujenga mashule, hospitali, barabara na kadhalika kwa kushirikiana na wanajamii kwa ujumla na/au pamoja na wafadhili mbalimbali.

Nawakaribisheni sana katika Mkoma Foundation ili kuiendeleza na iwe chombo cha kusaidia jamii kwa ujumla.

Ahsanteni sana

Dr. Wilson Mkoma

Mwenyekiti wa Foundation

 

This website was created for free with Own-Free-Website.com. Would you also like to have your own website?
Sign up for free